Maranatha
Kuombea Watu Wengine, Sura ya 30
Tena nawaambia wawili kati yenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 18:19. Mar 38.1
Nakumbuka kule Battle Creek kulipokuwa na wale waliokuwa na uchungu kwa ajili ya wale waliokuwa hawajaongoka, na wale waliokuwa gizani na walikuwa hawajaona nuru; mikutano ya maombi ilipangwa ili waifanye nguvu ya Mungu kuwa yao. Katika kila tukio viumbe wa mbinguni walishiriki katika juhudi hizi, na watu waliokolewa. Mar 38.2
Kama kuna idadi kubwa ya watu kanisani, hebu washiriki wagawanywe katika makundi, ili wafanye kazi si kwa ajili ya washiriki tu, lakini pia kwa ajili ya wasioamini. Kama mahali fulani kuna watu watu wawili au watatu tu wanaoujua ukweli, hebu wajikusanye na kuwa kikundi cha watenda kazi. Hebu wadumu kuwa na umoja, wakisonga mbele kwa umoja, kutiana moyo ili wasonge mbele, kila mmoja akipata shime na nguvu kutoka kwa wengine. Hebu waoneshe uvumilivu kama wa Kristo, bila kusema maneno kwa haraka bila kufikiri, wakitumia karama ya usemi kujengana katika imani takatifu. Na wafanye kazi katika upendo kama wa Kristo kwa ajili ya wale walio nje ya zizi. . . Kadiri wanavyofanya kazi na kuomba idadi yao itaongezeka. Mar 38.3
Kuna kazi ya umishenari wa nyumbani ambayo mahitaji kufanyika, ya tunasikia sauti ya kusishi, Kama kuna dhambi kiasi hiki na haja ya wafanyakazi katika nchi yetu wenyewe, kwa nini tunaonesha bidii sana kwa ajili ya nchi zingine? Huwa ninajibu, Shamba letu ni ulimwengu. . . Mwokozi aliwaagiza wanafunzi wake kuanzia kazi katika Yerusalemu, na kisha kwenda Yuda na Samaria, na hata mwisho wa ulimwengu. Watu wachache tu walilitiii fundisho hilo; lakini wajumbe walipeleka ujumbe kwa haraka kutoka sehemu moja hadi nyingine, wakipita katika nchi mbalimbali, wakiinua bendera ya injili katika sehemu za jirani na za mbali ulimwenguni. Lakini kulikuwa na kazi ya kujiandaa. Ahadi ya Mwokozi ilikuwa, “Lakini mtapokea nguvu, atakapowajia yule Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu.” Wale ambao hawatafuata mapenzi yao wenyewe, wakatafuta ushauri wa Bwana, hawatakuwa wasomi duni kwa kuwa Bwana atawafundisha. Mar 38.4