Maranatha
Miji Mikubwa Ifanyiwe Kazi Kutokea Nje, Sura ya 176
Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. 2 Wakorintho 6:17. Mar 184.1
Kama watu wa Mungu wazishikao amri, tunapaswa kuondoka kwenye miji mikubwa. Kama alivyotenda Henoko, tunapaswa kufanya kazi katika majiji lakini tusiishi ndani yake. Mar 184.2
Kadiri iwezekanavyo, taasisi ‘zetu zinapaswa kuwekwa mbali na majiji... Siyo mapenzi ya Mungu kwamba watu wake wakae ndani ya majiji, ambamo kuna ghasia na machafuko. Watoto wao na waepushwe na haya; kwani mfumo mzima umevunjwa na haraka, harara na kelele. Bwana anatamani kuwa watu wake wahamie mashambani, ambapo wanaweza kukaa katika nchi, na kuzalisha matunda yao wenyewe na mboga, ambapo pia watoto wao watakuwa. . . karibu na kazi za Mungu katika viumbe vya asili moja kwa moja. Ujumbe wangu ni huu: zitoeni familia zenu toka kwenye majiji. Mar 184.3
Sharti ukweli usemwe, bila kujali kama watu watausikia, au watauepuka. Majiji yamejazwa na majaribu. Tunapaswa kupanga kazi yetu kwa namna ambayo vijana wetu watawekwa mbali na uchafu huu kadiri iwezekanavyo. Mar 184.4
Majiji yanapaswa kufanyiwa kazi tukiwa katika vituo vya nje. Mjumbe wa Mungu alisema, “Je, majiji hayataonywa? Ndiyo; siyo kwa namna ya watu wa Mungu kuishi ndani yake, lakini kwa kuyatembelea, katika kuwaonya kuhusu kile kinachoijia dunia.” Mar 184.5
Wakati uovu unapoongezeka katika taifa, daima lazima isikike sauti ikitoa onyo na maelekezo, kama jinsi sauti ya Lutu ilivyosikika katika Sodoma. Hata hivyo Lutu angeweza kuokoa familia yake toka maovu mengi kama asingesogeza nyumba yake hadi ndani ya jiji hili ovu lililochafuka. Yote ambayo Lutu na familia yake waliyatenda pale Sodoma, wangeweza kuyatenda hata kama wangekuwa wameishi mahali mbali na jiji. Henoko alitembea na Mungu, na bado hakuishi ndani ya jiji lolote lililochafuliwa na kila namna ya vurugu na uovu, kama alivyokuwa Lutu ndani ya Sodoma. Mar 184.6
Yeye [Henoko] hakufanya makazi yake pamoja na waovu... Alijiweka pamoja na familia yake mahali ambapo mazingira yalikuwa safi kadiri ilivyowezekana. Kisha nyakati fulani alikwenda kwa wakazi wa dunia akiwa na ujumbe wake aliopewa na Mungu.... Baada ya kuutangaza ujumbe, daima alirejea mahali pake pa kupumzikia pamoja na baadhi ya wale waliokuwa wamepokea maonyo. Mar 184.7