Maranatha
Maandalizi kwa Kile Kilicho Mbeleni, Sura ya 153
“Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, nyie mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira BWANA.” Sefania 2:3. Mar 161.1
Uovu karibu umejaza kikombe chake. Dunia imejaa machafuko, na vitisho vikuu viko mbioni kuwapata wakazi wa dunia. Ule mwisho uko karibu sana. Watu wa Mungu wanapaswa kujiandaa kwa kile kilicho mbioni kuupata ulimwengu kwa jinsi ya ghafla ya kushtukiza. Mar 161.2
“Wakati wa taabu, ambao haujawahi kuwepo,” uko mbioni kutupata; nasi tutahitaji uzoefu tusiokuwa nao sasa na ambao wengi ni wavivu kuupokea leo. Daima mateso yanaonekana ni suala la kutarajiwa ila siyo halisi; ila hivyo sivyo ilivyo kuhusiana na zahama iliyoko mbele yetu. Kile nilichoonesha hakitoshi kuelezea uchungu mkali wa kipindi hicho. Mnamo wakati huo wa majaribu, kila nafsi sharti isimame peke yake mbele za Mungu. Mar 161.3
“Wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.” Eze. 14:20. Mar 161.4
Pambano Kuu la mwisho baina ya ukweli na uzushi siyo kitu kingine ila pambano la mwisho la ushindani mkuu uliopo dhidi ya sheria ya Mungu. Kupitia pambano hilo tunaingia katika pambano dhidi ya sheria za wanadamu na maagizo ya Yehova, kati ya dini ya Biblia na dini ya hekaya za wahenga na mapokeo ya wazee. Mar 161.5
Twapaswa kujifunza alama za njiani zenye kuelekeza kwenye nyakati tunazoishi. . . . Twapaswa kuomba kwa dhati kwamba tuweze kuandaliwa kwa mapambano ya ile siku kuu ya maandalizi ya BWANA. Mar 161.6
Wale wote ambao wanajisalimisha chini ya uongozi wa Mungu, wapate kuongozwa naye, watautambua mfuatano wa matukio yaliyoamriwa naye. Yakiwa yamevuviwa na Roho wake aliyeutoa uhai wake kwa ajili ya uhai wa ulimwengu, hawatasimama kidhaifu, wakielekeza vidole kwa yale wasiyoweza kuyatenda. Wakivalia silaha za Mungu, wataenda vitani, wakiwa tayari kuthubutu na kutenda kwa ajili ya Mungu, wakijua kuwa uweza wake usio na mwisho utawapatia mahitaji yao. Mar 161.7