Tangu Sasa Hata Milele
Kuokoka Toka Augsburg
Rafiki za Luther wakasihi sana kwamba hivi ilikuwa bure kwake kubakia, heri kurudi Wittenberg bila kukawia, na lile onyo halisi lifuatwe. Kwa hiyo akaondoka Augsburg kabla ya mapambazuko juu ya farasi, akisindikizwa na mwongozi moja tu aliyetolewa na mwamuzi. Kwa siri akafanya safari yake katika njia za giza za mji. Maadui, waangalifu tena wauaji, walikuwa wakifanya shauri la kumuangamiza. Nyakati hizo zilikuwa za mashaka na maombi ya juhudi. Akafikia mlango katika ukuta wa mji. Ulifunguliwa kwa ajili yake, na pamoja na mwongozi wake akapita ndani yake. Kabla mjumbe kupata habari ya safari ya Luther, alikuwa mbali ya mikono ya watesi wake Kwa habari ya kutoroka kwa Luther mjumbe akajazwa na mshangao na hasira. Alitumaini kupokea heshima kubwa kwa ajili ya mambo angatendea mtu huyu anaye sumbuake kanisa. Katika barua kwa Frederick, mchaguzi wa waSaxony, akashitaki Luther kwa ukali, kuomba kwamba Frederick amtume Mtengenezaji Roma ao amfukuze kutoka Saxony. TSHM 61.1
Mchaguzi alikuwa hajafahamu sana mafundisho ya mtengenezaji, lakini alivutwa sana kwa nguvu na usikivu wa maneno ya Luther. Frederick akaamua kuwa, mpaka wakati mtengenezaji atahakikisha kuwa na kosa. Frederick akawamlinzi wake katika jibu kwa mjumbe wa Papa akaandika: “Tangu Mwalimu Martino alipoonekana mbele yenu huko Augsburg, mungepashwa kutoshelewa. Hatukutumainia kwamba mungemulazimisha kukana bila kumsadikisha kwamba alikuwa na makosa. Hakuna wenye elimu hata mmoja katika utawala wetu aliyenijulisha ya kwamba mafundisho ya Martino yalikuwa machafu, yakupinga Kristo ao ya kupinga ibada ya dini.” Mchaguzi aliona kwamba kazi ya matengenezo ilihitajiwa kwa sisi akafurahi kuona mvuto bora ulikuwa ukifanya kazi yake katika kanisa. TSHM 61.2
Mwaka mmoja tu ulipita tangu Mtengenezaji alipoweka mabishano kwa mlango wa kanisa, lakini maandiko yake yaliamusha mahali pote usikizi mpya katika Maandiko matakatifu. Si kwa pande zote tu za Ujeremani, bali kwa inchi zingine, wanafunzi wakasongana kwa chuo kikuu. Vijana walipokuja mbele ya Wittenberg kwa mara ya kwanza “wakainua mikono yao mbinguni, na kusifu Mungu kwa kuweza kuleta nuru ya ukweli kuangaza kutaka mji huu.” TSHM 61.3
Luther alikuwa amegeuka nusu tu kwa makosa ya kanisa la Roma. Lakini aliandika, “Ninasoma amri za maaskofu, na ... sijui kama Papa ndiye anayekuwa mpinzani wa Kristo yeye mwenyewe, ao mtume wake, zaidi ya yote kristo ameelezwa vibaya kabisa na kusulubiwa ndani yao.” TSHM 61.4
Roma ikazidi kukasirishwa na mashambulio ya Luther. Wapinzani washupavu, hata waalimu (docteurs) katika vyuo vikuu vya Kikatoliki, wakatangaza kwamba yule angeweza kumua mtawa yule angekuwa bila zambi. Lakini Mungu alikuwa mlinzi wake. Mafundisho yake yakasikiwa po pote--“katika nyumba ndogo na nyumba za watawa (couvents), ... katika ngome za wenye cheo, katika vyuo vikubwa, katika majumba ya wafalme.” TSHM 62.1
Kwa wakati huu Luther akaona ya kwamba ukweli mhimu juu ya kuhesabiwa haki kwa imani ilikuwa ikishikwa na Mtengenezaji, Huss, wa Bohemia. “Tumekuwa na vyote” akasema Luther, “Paul, Augustine, na mimi mwenyewe, Wafuasi wa Huss bila kujua!” “ukweli huu ulihubiriwa ... karne iliyopita na ikachomwa!” TSHM 62.2
Luther akaandika basi mambo juu ya vyuo vikuu: “Ninaogopa sana kwamba vyuo vikuu vitaonekana kuwa milango mikubwa ya jehanumu, isipokuwa vikitumika kwa bidii kwa kueleza Maandiko matakatifu, na kuyakaza ndani ya mioyo ya vijana. ... Kila chuo ambamo watu hawashunguliki daima na Neno la Mungu kinapaswa kuharibika.” TSHM 62.3
Mwito huu ukaenea po pote katika Ujermani. Taifa lote likashituka. Wapinzani wa Luther wakamwomba Papa kuchukua mipango ya nguvu juu yake. Iliamriwa kwamba mafundisho yake yahukumiwe mara moja. Mtengenezaji na wafuasi wake, kama hawakutubu, wangepaswa wote kutengwa kwa Ushirika Mtakatifu. TSHM 62.4