Tangu Sasa Hata Milele

39/257

Kazi ya Luther Inaanza

Sauti ya Luther ikasikiwa mimbarani katika onyo la kutisha. Akaweka mbele ya watu tabia mbaya sana ya zambi na kufundisha kwamba haiwezekani kwa mtu kwa kazi zake mwenyewe kupunguza zambi zake ao kuepuka malipizi yake. Hakuna kitu bali toba kwa Mungu na imani katika Kristo inaoweza kuokoa mwenye zambi. Neema ya Kristo haiwezi kununuliwa; ni zawadi ya bure. Akashauri watu kutokununua vyeti vya huruma, bali kutazama kwa imani kwa Mkombozi aliyesulubiwa. Akasimulia juu ya habari mambo ya maisha yake ya uchungu na akahakikisha wasikilizaji wake kwamba kwa kuamini Kristo ndipo mtu atapata amani na furaha. TSHM 56.3

Wakati Tetzel alipoendelea na kiburi chake cha kukufuru, Luther akajitahidi kusema kutokukubali kwake. Nyumba ya kanisa la Wittenberg ilikuwa na picha (reliques) ambayo kwa sikukuu fulani yalionyeshwa kwa watu. Maondoleo kamili ya zambi yalitolewa kwa wote waliozuru kanisa na waliofanya maungamo. Jambo moja la mhimu sana la nyakati hizi, sikukuu ya Watakatifu Wote, ilikuwa ikikaribia. Luther, alipoungana na makundi yaliyo jitayarisha kwenda kanisani, akabandika kwa mlango wa kanisa mashauri makumi tisa na tano juu ya kupinga ya uuzishaji wa vyeti (musamaha). TSHM 57.1

Makusudi yake yakavuta uangalifu wa watu wote. Yakasomwa na kuyakariri po pote, yakasitusha sana watu katika mji wote. Kwa maelezo haya yalionyeshwa kwamba uwezo kwa kutoa masamaha ya zambi na kuachiliwa malipizi yake haukutolewa kwa Papa ao kwa mtu ye yote. Ilionyeshwa wazi wazi kwamba neema ya Mungu ilitolewa bure kwa wote wanaoitafuta kwa toba na imani. TSHM 57.2

Mambo yaliyoandikwa na Luther yakatawanyika pote katika Ujeremani na baada ya majuma machache yakasikilika pote katika Ulaya. Wengi waliojifanya kuwa watu wa kanisa la Roma wakasoma mashauri haya (mambo yalioandikwa na Luther) kwa furaha, kutambua ndani yao sauti ya Mungu. Walijisikia kwamba Bwana aliweka mkono wake kufunga maji yaliyotomboka ya uovu ulioletwa kutoka kwa Roma. Waana wa wafalme na waamuzi kwa siri wakafurahi kwamba kizuio kilipashwa kuwekwa juu ya mamlaka ya kiburi ambayo ilikataa kuacha maamuzi yake. TSHM 57.3

Wapadri wa hila, kuona faida zao kuwa hatarini, wakakasirika. Mtengenezaji (Reformateur) alikuwa na washitaki wakali wakushindana naye. “Nani asiyejua, ” akajibu, “kwamba si mara nyingi mtu kuleta mawazo mpya bila. kushitakiwa kukaamsha mabishano? ... Sababu gani Kristo na wafia dini wote waliuawa? Kwa sababu ... walileta mambo mapya bila kupata kwanza shauri la unyenyekevu la mtu wa hekima na maoni ya zamani.” TSHM 57.4

Makaripio ya adui za Luther, masingizio yao juu ya makusudi yake, mawazo yao ya uovu juu ya tabia yake yakawajuu yake kama garika. Alikuwa ameamini kwamba waongozi watajiunga naye kwa furaha katika matengenezo. Mbele ya wakati aliona siku bora zikipambazuka kwa kanisa. TSHM 57.5

Lakini kutiia moyo kukageuka kuwa karipio. Wakuu wengi wa kanisa na jamii ya watu wa serkali kwa upesi wakaona kwamba ukubali wa mambo haya ya kweli karibu ungaliharibu mamlaka ya Roma, kuzuia maelfu ya vijito vinavyotiririka sasa katika nyumba ya hazina yake, na vivi hivi kupunguza anasa ya waongozi wa Papa. Kufundisha watu kumutazama Kristo peke yake kwa ajili ya wokovu kungeangusha kiti cha askofu na baadaye kuharibu mamlaka yao wenyewe. Kwa hiyo wakajiunga wao wenyewe kupinga Kristo na kweli kuwa wapinzani kwa mtu aliyetumwa kwa kuwaangazia. TSHM 57.6

Luther akatetemeka wakati alipojiangalia mwenyewe--mtu mmoja akapinga watu wa nguvu nyingi wa dunia. “Mimi nilikuwa nani?” akaandika, “kupinga enzi ya Papa, mbeie yake ... wafalme wa dunia na ulimwengu wote ulitetemeka? ... Hakuna mtu anaweza kujua namna gani moyo wangu uliteseka mda wa miaka hii miwili ya kwanza na katika kukata tamaa, naweza kusema katika kufa moyo, nilizama.” Lakini wakati usaada wa kibinadamu ulishindwa, alitazama kwa Mungu peke yake. Aliweza kuegemea katika usalama juu ya ule mkono ulio wa guvu zote. TSHM 58.1

Kwa rafiki Luther akaandika: “Kazi yako ya kwanza ni kuanza na ombi. ... Usitumaini kitu kwa kazi zako mwenyewe, kwa ufahamu wako mwenyewe: Tumaini tu katika Mungu, na katika mvuto wa Roho Mtakatifu.” Hapa kuna fundisho la maana kwa wale wanaojisikia kwamba Mungu amewaita kutoa kwa wengine ibada ya dini ya kweli kwa wakati huu. Katika vita pamoja na mamlaka ya uovu kunakuwa na mahitaji ya kitu kingine zaidi kuliko akili na hekima ya kibinadamu. TSHM 58.2