Hatua Za Ukamilifu Katika Kristo
Sura ya Kumi ya Mbili—YATUPASAYO KUFANYA TUNAPOKUWA NA MASHAKA MOYONI
Watu wengi, hasa walio Wakristo wapya, siku nyingine huwa na mashaka moyoni juu ya mambo mengine katika Biblia ambayo hawawezi kuyaeleza ama kufahamu. Naye Shetani huyatumia mambo yale kwa kuwapunguzia imani yao katika kukubali kwamba Biblia ni ufunuo wa Mungu. Wasema,“Nawezaje kujua njia iliyo ya haku ? Kama kweli Biblia ni Neno la Mungu, nawezaje kuondolewa mashaka haya moyoni, nisi je kushikwa na fadhaa ?” HUK 47.1
Kila jambo atakalo Mungu tulisadiki, hakosi kutubainishia sababu ya kuwa na imani juu ya jambo lile. Jinsi Mungu mwenyewe alivyo hai, namna ya tabia zake, na ukweli wa Neno lake, mambo haya yote yamehakikishwa kwetu kwa namna nyingi. Hata hivyo Mungu haoni ni afadhali kutuondolea nafasi ya kuwa na shaka. Imetupasa kumwamini Mungu kwa vile tunavyobainishiwa mioyoni mwetu juu ya mambo yasiyoonekena, siyo kwa ajili ya mambo yaliyo dhahiri katika macho yetu ya kibinadamu. HUK 47.2
Haiyamkiniki kwa nia ya kibinadamu kufahamu kabisa namna za tabia za Mungu wala kazi yake. “Kwa kutafuta utampata Mungu ? Utampata Mwonyiozi Mungu alivyo bora ? Juu kama mbingu; utafanyaje ? Chini kupita ahera; utajuaje ?” Ayub 11:7,8. HUK 47.3
Mtume Paulo alisema, “Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hata kiasi! hukumu zake hazichunguziki na njia zake hazitafutikani” Warumi 11:53. Na hata “mawingu na giza yamemzunguka,” “haki na hukumu maweko ya kiti chake.” Zab.97:2. Katika matendo yake juu yetu twaweza kufahamu makusudi yake kutosha kuona upendo Wake na huruma yake isiyo na kiasi, na jinsi uwezo wake usivyo cheo. Twaweza kutambua makusudi yake kwa kadiri inavyotufaa; zaidi ya hayo imetulazimu kutawakali Mwenyiezi Mungu, ambayo moyo wake umejaa upendo. HUK 47.4
Katika Neno la Mungu, vilevile katika sifa yake, kuna mambo ya siri wasiyoweza wanadamu kuyafahamu. Jinsi dhambi ilivyoingia ulimwenguni, jinsi Kristo alivyofanyika kuwa na umbo halisi la binadamu, uzazi wa pili jinsi ulivyo, ufufuo, na mengineyo katika Biblia, ni mafumbo makubwa sana kushinda akiii za kibinadamu kuyaeleza, wala kuyafahamu maana yake vizuri. Lakini hatuna sababu ya kuwa na shaka juu ya Neno la Mungu kwa ajili ya kutofahamu mafumbo ya maongozi yake na majaliwa yake Mungu. Hata katika mambo ya ulimwengu na viumbe vyake twaona mafumbo mengi tusiyowoza kuyafahamu. Wenye akili sana wameshindwa kueleza habari za uhai jinsi ulivyo, hata uhai wa vidudu vidogo. Mahali pote pana maajabu tusiyoweza kuyafahamu. Kwa hivyo mbona tunastaajabu tukiambiwa kuwa kuna mambo ya kiroho yasiyoweza kufahamiwa na kuelewa na binadamu ? Shida imekuwa kwa ajili ya udhaifu na akili chache ya binadamu. Katika Maandiko yenyewe Mungu ametuhakikishia jinsi Maandiko haya yalivyo ya Mungu, tusione shaka moyoni juu ya Neno lake kwa sababu ya kutofahamu mafumbo yake yote. HUK 47.5
Mtume Petro amesema kwamba katika Maandiko “yamo mambo ambayo ni vigumu kurlewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa....kwa upotevu wao wenyewe.” 2 Pet.3:16. Wengine husema kwamba mafumbo ya Biblia ni sababu ya kutosadiki maneno yake; lakini kwa kweli mafumbo haya ni ushahidi mkuu kuwa yametoka kwa Mungu. Kama ingekuwa Biblia haina habari za Mungu ila tu mambo yawezayo kuelewa kwa urahisi na kufahamiwa na binadamu, Biblia isingekuwa na hakika kwamba ni ya Mungu kweli. HUK 48.1
Mafundisho ya Biblia juu ya wokofu, yametolewa kwa namna ifaayo kwa mahitaji na matakwa ya moyo wa binadamu; watu wastaarabu na wenye elimu nyingi wamevutwa na uzuri wa maneno yake; na hata watu duni waweza kuolowa na kufahamu njia ya wokofu.Hata hivyo twaweza kuyasadiki hivi tu, kwa kuwa Mungu ndiye anayetujulisha manbo hayo. Mpango wa Mungu juu ya ukombozi wa wanadamu umebainishwa vizuri kwetu, ili mtu ye yote ajue la kufanya katika kutubia kwa Mungu, na kuwa na imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo, apate kuokoka kwa njia aliyoiweka Mungu. Walakini ndani ya mambo haya kuna mafumbo ya Mungu yasiyofunuliwa ila kwa yule anayeyachunguza kwa moyo na bidii. Na kwa jinsi anavyozidi kuyachunguza naneno ya Biblia, ndivyo anavyozidi kusadikishwa kwamba ni Neno la Mungu aliye hai. HUK 48.2
Wenye kumkana Mungu hutupia mbali Neno la Mungu kwa sababu hawawezi kufahamu nafumbo yake yote. Hata na wengine wanaojidai kuwa hisadiki Biblia, huona mashaka moyoni juu ya jambo hilo. Mtume amesoma, “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Waeb.3:12. Ni vizuri kujifunza mafundisho ya Biblia, na kuchunguza “hata mafumbo ya Mungu,” (I Wakor.2:I0), kwa kadiri yanavyofunuliwa katika Maandiko. Ingawa ni “kwa Bwana Mungu wetu yaliyo ya siri,” ni kwetu sisi “yaliyofunuliwa.” Kumbu.29:29. Lakini ni kusudi la Shetani kuipotoa njia ya binadamu kama anataka ku-yachunguza mambo. Kwa ajili ya ufundi wanaojiona kuwa nao katika kuchunguza mafundisho ya Biblia, watu wengine huwa wepesi wa kuchukizwa wasipoweza kueleza maana ya kila sehemu ya Maandiko kwa namna ya kutosheleza nafsi zao wenyewe. Ni aibu kwao kukiri kwamba hawayafahamu vizuri. Hawataki kumngo jea Mungu hata atakapowafunulia maana ya hakika. Huona kwamba akili za kibinadamu zimetosha kuwafahamisha Maneno ya Mungu; nao wakishindwa kufanya hivi, basi, huyakana kuwa si ya Mungu. Kuna maelezo na mafundisho mengi ya dini yanayodhaniwa tu ya kuwa asili yake ni maneno ya Biblia, lakini maana yake ni kinyumo kabisa cha ukweli wa Biblia. Kwa ajili ya mambo haye watu wengi hushikwa na fadhaa na huona shaka mioyoni mwao. Lakini imekuwa hivyo si kwa ajili ya Neno la Mungu hasa, ila kwa kuwa wanadamu wamepotoa naneno yake. HUK 48.3
Kama wanadamu wangeweza kupata kufahamu Mungu jinsi alivyo hasa, pamoja na natendo yake, basi, wasingekuwa na jambo jipya la kuvumbua, wasingezidi kuelinishwa tena, wasingepata kuzidisha maondeleo yao ya kiroho. Hapo Mungu asingekuwa Mwenye enzi; tena kwa vile ambavyo binadamu angekuwa amefika mwisho wa elimu na maarifa yote, asingepata maendeleo yo yote tena. Tumshukuru Mungu kwa kuwa sivyo hivyo. Mungu ni mwenye uwezo wote, mwenye kujua yote; “ndani yake zimo hazina zote za hekima na maarifa.” Wekor.2:3. Maisha na nilele wanadanu watakuwa wenachunguza na kuendelea kufahanu akili za Mungu, wema wake, na enzi yako, bila nwisho. HUK 49.1
Kuna njia moja tu kwa kupata kuelimishwa na kuendelea ku-fahamu Neno la Mungu, - kama Roho ya Mungu inanglaa mioyoni nwetu na kutumiliki. “Mambo ya Mungu hakuna ayajuaye ila Roho ya Mungu;” “maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” 1 Wakor.2:11,10. Tena Mwokozi aliwaahidia wafuasi wake hivi, “Ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli;...atatwaa katika iliye yangu, atawapasheni habari.” Yoh.16:13,14. HUK 49.2
Mungu ataka binadamu atumie akili zake; na kuchunguza na kujifunza Biblia kutaimarisha na kuadilisha roho na nia zetu kwa jinsi isivyowezekana katika kujifunza nanbo yo yote mengine. Ili tupate kufahamu Msandike , na mioyo yetu isifadhaishwe inetupasa kuwa na imani na moyo mmo ja kama watoto, tayari kufundishwa na kumwomba Roho Mtakatifu msaada wake. Tukiona uwezo wa Mungu na akili zako jinsi viliyo kuu zaidi pasipo kiasi, na kuelewa hali yetu ya kutoweza kufahanu namna ya utukufu wake, hapo basi inetupasa kunyenyekea; na tunapofunua kitabu cha Neno lake, imetupasa kuwa na heshima na unyenyekevu moyoni kama tulio mbelo yake hasa. HUK 49.3
Kuna nanbo mengi ya fumbo, ambayo Mungu atawadhihirishia wale watakao kweli kuyafahamu. Lakini bila uongozi wa Roho Mtakatifu binadamu huelekea kupetoa maneno ya Biblia na kueleza maana isiyo ya kweli. Masomo nengi ya wanadanu katika Biblia yanekuwa bure bila faida. Kana kitabu cha Neno la Mungu kinafunuliwa bila heshima na maombi: mtu asipomkazia Mungu fikara zake na upendo wake na kufanya napenzi ya Mungu, bila shaka atashikwa na fadhaa. Ndipo Shetani atamtawala mawazo yake, na kumtia moyoni mwake maelezo ya Biblia yasiyo ya kweli. Kila mara wanadanu wasipopatana na Mungu katika maneno na matendo yao, ingawa ni wenye naarifa ya namna gani, bila shaka watakosa kufahanu Maandiko, tena haifai kuwaamini maelezo yao. Wengi wao walio na mashaka moyoni, asili ya kushuku kwao ni kupenda dhanbi. Masharti na vizuizi vya Neno la Mungu havipendezi wenye moyo wa kujisifu, na wale wasiokubali kufanya matakwa ya Biblia lake huwa wepesi kutosadiki kuwa ni Neno la Mungu halisi. Bali, wote watakao kwa noyo kujua matakwa ya Mungu na kuyafanya, hao nao watabainishiwa kuwa Biblia ni Maneno ya Mungu yawezayo kuwapa hekima hata wapate wokofu. Kristo asema,“Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu.” Yoh,7:17. Badala ya kubishana bure juu ya mambo msiyoweza kuyafahamu, heri mfanye kila wajibu wenu kwa vile mnavyofahamu na kuelewa navyo, ndipo mtasaidiwa kuyafahamu na kuyafanya yale ambayo sasa mnayaonea mashaka. HUK 49.4
Mungu ataka tujihakikishie ukweli wa Neno lake na ahadi zake. Asema, “Onjeni mwone BWANA ndiye mwema.” Zab.34:3. Tusitegemee neno la wengine, ila tuonje sisi wenyewe na kuona wema wake. Asema tena, “Ombeni, na mtapata.” Yoh.16:24. Ahadi zake zitatimia. Haziwezi kuwa na upungufu. Wa kwa vile tunavyomkaribia Yesu, na kufurahiwa na upendo wake, ndivyo nuru yako itakavyong aa mioyoni mwetu, tena mashaka na giza vitaondolewa. Mtume Paulo asema kwamba Mungu alituokoa “na nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.” Wakol.1:13. Kila ambaye “amepita toka mauti hata uzima” anawoza kutia “muhuri yake kwamba Mungu ni kweli.” Yoh.5:24; 3:33. Aweza kushuhudia,“Nimopata msaada kwake Yesu; nayo ameniruzuku mahitaji yangu yote, nimetoshewa njaa ya moyo wangu; tena sasa Biblia inakuwa kwangu ufunuo wa Yesu Kristo. Waniuliza mbona namwamini Yesu ? - Kwa kuwa ni Mwokozi wangu. Kwa nini nasadiki Biblia ? - Kwa sababu nimeona kuwa ni sauti ya Mungu moyoni mwangu.” Twawoza kuwa na ushuhuda ndani yetu kuwa neno la Biblia ni kwoli, tena Kristo ni Mwana wa Mungu. Twajua kwamba hatufuati hadithi zilizotungwa kwa werevu. 2 Petro 1:16. HUK 50.1
Petro awaamuru Wakristo ndugu zake, “Kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wotu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.” 2 Pet.3:l8. Watu wa Mungu wakikaa katika neema yake, watazidi kudhihirishiwa Neno lake. “Matembezi yao wenye haki kama nuru nyeupe, iangazayo ikizidi hata mehana utimiapo.” Methali 4:18. HUK 50.2
Kwa imani twaweza kutazama mbole hata kwa ufalme wa Mungu, na kutumaini ahadi ya Mungu juu ya kutuzidisha akili, na jinsi uwezo wetu woto utakavyoungamana na, uwezo wa Mungu. Twaweza kufurahi kwa kuwa yoto ambayo sasa tumeshikwa na fadhaa nayo, hapo ndipo yatadhihirishwa kwetu; mambo yanayokuwa magumu kufahamiwa, wakati huo yataelezwa dhahiri. “Wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.” 1 Wakor.l3:12. HUK 50.3
Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa:
Kukubali Neno lake nina raha moyoni,
Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kwake daima napata uzima na amani.
Nafurahi kwa sababu nimekutegemoa;
Yosu, Mpendwa na Rafiki, uwe nami daina.
HUK 50.4