Hatua Za Ukamilifu Katika Kristo

6/13

Sura ya Sita—KUMWAMINI MUNGU NA KUKUBALIWA NAYE

Kwa jinsi dhamiri na roho yako vilivyohuishwa na Roho Mtakatifu, hivyo uanazidi kufahamu abaya wa dhambi, nguvu zake, na jinsi inavyoleta taabu; tera unazidi kuchukizwa nayo moyoni. Huona kwamba kwa ajili ya dhambi umepata kutengwa na Mungu, nawe umekuwa umefungwa na uovu. Huwezi kamwe kujisaidia mwenyewe. Nia yako si safi, tena moyo wako huwa najisi. Umefahamu kwamba maisha yako hujaa dhambi na mambo ya kujipendeza nafsi yako mwenyewe. Wataka sana kusamehewa makosa yako, upate kutakaswa na kuwekwa huru kutoka utumwa wa Shetani. Kupatana na Mungu, na kufanana naye, na kuwa salama moyoni, - waweza kufanya nini ili uwe katika hali hiyo ? HUK 21.1

Hali hii haiwezi kununuliwa kwa fedha, pia haipatikani kwa ajili ya akili wala elimu; tena huwezi kutumaini kuwa katika hali hiyo kwa juhudi zako mwenyewe. Bali utaipata bure mkononi mwa Mungu kama karama yake, “pasipo fedha na pasipo thamani.” Isa.55:1. Ni juu yako tu kuichukua. Mungu asema, “Dhambi zenu zikiwa kama bendera (nyekundu), zitakuwa nyeupe kama theluji; zikiwa nyekundu nyekundu mno, zitakuwa kama sufu.” Isa.1:18. “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, roho mpya nitatia ndani yenu.” Ezek.36:26. HUK 21.2

Basi, umeziungama dhambi zako na kuziwekea mbali kwa moyo wako. Pia umeazimia kujitoa kuwa mtu wa Mungu. Sasa nenda kwako, na kumwomba ili akusafishe dhambi zako zote, akukupe moyo mpya. Ndipo usadiki kwamba amefanya hivyo kwa kuwa ndivyo alivyoahidi.Yesu alipokuwa hapa duniani, alitoa fundisho lile, kwamba imetulazimu kusadiki ya kuwa tumepata upaji wa Mungu aliotuahidi, ndivyo itakavyokuwa wetu. Yesu aliwaponya watu maradhini mwao walipomwamini uwezo wake. Aliwasaidia katika mambo waliyoweza kuyaona na macho ya kimwili, ili wapate kumtumainia juu ya mambo wasiyoweza kuyaona - yaani, wapate kusadiki uwezo wake katika kuwasamehe dhambi zao. Hivyo ndivyo alivyosema katika kumponya yule mgonjwa wa kupooza:“Ili mjue ya kuwa Mwana wa Adamu yuna mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza), Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende nyumbani kwako.” Mattayo 9:6. Mtume Yohana pia, aliposema juu ya miujiza ya Kristo, alisema hivi, “Hizi zimeandikwa mpata kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.” Yoh.20:31. HUK 21.3

Hivyo tukisoma habari katika Biblia jinsi Yesu alivyoponya wagonjwa wa kimwili, twaweza kufundishwa na kufahamu namna ya kumsadiki kuwa kweli anaweza kuachilia na kuondoa dhambi. Tusome juu ya yule mgonjwa wa kupooza. Alikuwa hoi kwa ugonjwa tangu miaka thelathini na minane, asipoweza kwenda kwa miguu. Walakini Yesu alimwambia, “Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende.” Yule mgonjwa angaliweza kusema, Bwana, kama utaniponya, nitafanya usemavy.” Lakini sivyo. Alikubali neno la Kristo, alisadiki kwamba amepona, akajitahidi mara moja; alifanya jinsi Kristo alivyomwamuru, ndipo Mungu akamytolea nguvu zake, naye ngonjwa akapona mara, akawa mtu mzima. HUK 21.4

Hivyo ndivyo wewe u mwenye dhambi. Huwezi kulipia ukosefu wako, huwezi kugeuza moyo wako na kujitakasa mwenyewe kuwa safi. Lakini Mungu ameahidi kwamba atakufanyia hivyo katika Kristo. Unakubali hivyo. Na kwa jinsi unavyoziungama dhambi zako, na kujitoa kwa Mungu na kuazimia kumtumikia, ndivyo Mungu atakavyotekeleza ahadi yake, nawe utaachiliwa dhambi na kutakaswa; na utakuwa mtu mzima jinsi yule mgonjwa wa kupooza alivyowezeshwa na Kristo kwenda kwa miguu mara aliposadiki kwamba amepona. Ikiwa unaamini kama yule, ndivyo utakavyopata kupona kwa dhambi. HUK 22.1

Yesu asema, “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:24. Lakini kuna masharti juu yetu ili ahadi hii itimizwe, - tuombe kama vile apendavyo Mungu. Tena ni mapenzi ya Mungu kuziondclea dhambi zetu na kututakasa, ili tuwe watoto wake na kuishi maisha yaliyo safi kwa uwezo wake Mungu. Kwa hiyo twaweza kumwomba Mungu mibaraka hii, na kuamini kwamba tumeipata, na kumshukuru Mungu kwa kuwa kweli tumeipata mibaraka yake. Ni jambo linalotuhusu, kwenda kwake Yesu na kutakaswa, na kuhesabiwa kuwa ni safi bila lawama, na pasipo kuaibishwa. “Sasa, basi, hapana hukumu juu yalo walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya Roho.” Warumi 8:1. HUK 22.2

Toka sasa mwili wako si wako mwenyewe; umenunuliwa na bei kubwa. “Hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu,....bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo, aliyejuliwa tangu zamani.” 1 Petro 1:18-20. Kwa kumwamini Mungu tu, Roho Mtakatifu ameanzisha uzima upya moyoni mwako. Sasa umekuwa kama mtoto aliyezaliwa kwa kiroho kuwa katika watu wa nyumba ya Mungu, naye anakupenda namna apendavyo Mwana wake. HUK 22.3

Sasa kama umejitoa kuwa wa Yesu, usirudi nyuma tena kutoka mkononi mwake. Kila siku heri useme, “Mimi ndimi wako Kristo; nimejitoa kwake;” tena ukamwomba Roho yake akulinde kwa neema yake. Ulipata kuwa mtoto wa Mungu kwa njia ya kujitoa kwake na kumwamini; hivyo ndivyo utakavyofanya kila siku ili uishi katika Kristo. “Basi, kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye.” Wakol.2:6. HUK 22.4

Wengine hufikiri kwamba ni lazima kuwa na wakati wa kujaribiwa na kumdhihirishia Mungu ya kuwa wameongoka kabla ya kuweza kupata mibaraka yake. Lakini sivyo. Waweza kupata mbaraka wa Mungu mara. Lazima wawe na Roho ya Kristo mioyoni mwao, kuwasaidia udhaifu wao katika kushindana na maovu. Yesu apenda ili twende kwake jinsi tulivyo, - wenye dhambi, wadhaifu, wasioweza kujiokoa wenyewe. Hata kama tumefanya mabaya ya namna gani, tusiogope kufika kwake, Atatupokoa kwa moyo wa upendo, naye anakubali kututakasa makosa na unajisi wo wote. HUK 22.5

Wengi huanguka katika neno hili: hawaamini kwamba Yesu anawasamehe wao wenyewe hasa. Hawakubali ya kuwa jinsi Mungu asemavyo, ndivyo ilivyo. Ni haki ya watu wote wanaoyatimiza masharti ya Mungu, kujua kwa hakika kwamba kuna masamaha kwa kila dhambi. Ahadi za Mungu ni kwa kila mkosaji mwenye kutubu. Hata mwenye kufanya dhambi iwayo yote, hakuna asiyeweza kupata nguvu, na usafi na kuwa mwenye haki katika Kristo Yesu aliyekufa kwa ajili yetu. Huwaambia waishi, na wasife. HUK 23.1

Mungu hatutendei jinsi binadamu huwatendea wenzake. Yu mwenye rehema, upendo na huruma. Asema, “aache mwovu njia yake, na mtu mbaya mawazo yake; akamrudie BWANA, naye atawarehemu; na kwa Mungu wetu, kwani mkarimu kuachilia.” “Nimefuta, kama wingu zito, makosa yako, na, kama wingu, dhambi zako.” Isa.55:7; 44:22. HUK 23.2

“Kwani sikifurahii kifa chake afaye, anena Bwana Mungu: basi geukeni, mkaishi.” Ezek,18:32. Shetani yu tayari kila mara kutudanganya ya kwamba ahadi za Mungu si ya watu kama sisi.Lakini tusisikilize maneno yake, bali tuseme hivi moyoni: Yesu alikufa kwa ajili yangu, niwe na uzima, Anipenda mimi; ataka nisife. Baba yangu aliye mbinguni ni mwenye huruma; na hata nimemtendea vibaya, na ingawa nimepoteza mibaraka yake kwa siku zilizopita, kwa vile upendo anavyonipenda, nitaondoka na kwenda kwake Baba na kusema, “Baba, nimekosa juu ya mbingu, na mbelo yako; sistahili kuitwa mwana wako baada ya hayo: unifanye kuwa kama mmojawapo wa watumishi wako.” Mfano ule wa Mwana Mpotevu huonyesha namna Mungu anavyowapokea wanaokuja kwake: “Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona, akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni, akambusu sana.” Luka 15:18-20. HUK 23.3

Na hata mfano huu umepungukia kuonyesha sawa namna ya upendo na huruma wa Baba aliye mbinguni, kwa kuwa huruma wake haina kifani. Mungu asema, “Kupenda nimekupenda mapenzi ya milele; kwa hiyo na wema nimekuvutia.” Yer.31:3. Mwenye dhambi angali akawa mbali na Baba yake, yule Baba anamhurumia moyoni mwake na kumtaka sana. Na kila mpotevu asikiaye moyoni mwake kwamba anataka kumrudie Mungu, ameona hivyo kwa kuwa Roho Mtakatifu anamvuta kwa Baba ampendaye sana. HUK 23.4

Kama umeyajua ahadi njena za Mungu zilizoandikwa katika Biblia, wawezaje kuona mashaka moyoni ? Wawezaje kudhani kwamba Mungu angemzuia mwenye kumfikilia na kutubu ? Fikara kama hizi ziondolewe mbali kabisa! Katika kumdhania Baba yetu hivi, unajihatarisha moyo wako mwenyewe. Ni kweli kama Mungu huchukizwa na maovu, lakini hupenda mwanadamu mpotevu, hata akajitoa pamoja naye Kristo, ili aliye yote amwaminiye apate kuokoka na kurithi urithi wa milele katika ufalme wake utukufu. Angeweza kusema nini tena zaidi ya hayo aliyoyasema kwa kuonyesha jinsi anavyotupenda sisi ? Asema, Aweza mwanamke kusahau mtoto wake anyonyaye, asomrehemu mwana wa tumbo lake ? hata waweza hawa kusahau, ila siwezi mimi kusahau wewe.” Isa.49:15. HUK 23.5

Inueni macho, ninyi mlio na mashaka na wenye kuogopa; Yesu ndiye Mwombezi wetu. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mwanawe Mpendwa, na kumwomba msaada wake ili isionekane kwamba kufa kwake Yesu kumekuwa bure kwako. Roho Mtakatifu anakuita hivi leo. Mtolee Yosu moyo wako mzima, upate mbaraka wake. HUK 24.1

Nawe ukisoma ahadi zake, kumbuka kwamba yote husemwa kwa upendo na huruma. “Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi kwa wingi wa neema yake.” Waef.l:7. Ndiyo, usadiki tu ya kuwa Mungu ni msaidizi wako. Anataka kuwarudisha wanadamu katika hali yao ya kwanza, kwa jinsi alivyowaumba kwa mfano wake Mungu. Nawe ukimkaribia Mungu na kuziungama dhambi zako na kutubu, yeye pia atakukaribia kwa moyo wa rehema na masamaha. HUK 24.2

Nitwao hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu, sasa naja.

Hivi nilivyo; si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisameho dhambi zangu,
Bwana Yesu, sasa naja.

Nawe hivi utanitwaa;
Nisisubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu, sasa naja,

Hivi nilivyo; mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu, sasa naja.
HUK 24.3